KUHUSU OKOA MOMBASA
KUHUSISHA UMMA KWA RASILIMALI ZA UMMA
Okoa Mombasa ni muungano wa vyama vya wafinyakazi, wafanyibiashara, Wataalamu mbalimbali na mashirika zisizo za kiserikali kwa minajili ya kujali maswala ya riziki na ustawi wa wakaazi wa Mombasa
Lengo letu kuu na kauli mbiu ni: Kuwashirikisha wakaazi kwa matumizi ya rasilimali za kaunti.kama kauli au sera itaathiri wakaazi wa Mombasa na pwani kwa jumla basi nilazima wahusishwe kikamilifu na matakwa yao kuzingatiwa.
Je, malengo yetu tunayafikia vipi?
Tunatetea haki ya upatikanaji wa habari, kukusanyika kwa amani na kushiriki kama ilivyoashiriwa katika Katiba ya Kenya 2010. Tunafuatilia mafanikio ya ugatuzi katika Kaunti ya Mombasa na kwa ushirikiano na wengine.
Je, tunashughulikia maswala yapi?
Tangu 2019, tumeshughulikia mipango kadhaa inavyoathiri Pwani, ikiwa ni pamoja na agizo la kulazimisha usafirishaji wa mizigo kutumia Reli ya Standard Gauge, jaribio la ubinafsishaji wa Bandari ya Mombasa, na kampeni ya kubadilisha jina la bustani la mama ngina water front.
Tazama
Okoa Mombasa mwanzilishi mwenza Khelef Khalifa anajadili dhamira na malengo ya muungano.
SOMA PAMPHLE ZETU
Pata maelezo zaidi kuhusu Okoa Mombasa, kile tunachofanya na tunachopigania.
MASHIRIKA YA MWANACHAMA
Muslims for Human Rights (MUHURI)
Kenya Transporters Association (KTA)
Dock Workers Union Kenya
Kenya Long Distance Truck Drivers' Union
Haki Yetu Organisation
Fast Action Summit
InformAction
Ajenda Kenya
Human Rights Watch
Taireni Association of Mijikenda
Stella Maris International
Shakirina Youth for Development
Road Hauliers Association of Kenya
Pata habari, shiriki!
Jiunge na orodha yetu ya utumaji barua za mara kwa mara kuhusu masuala zinazoathiri Mombasa na Pwani.